Saturday, January 17, 2026
spot_img
HomeKiswahili newsSERIKALI YAKANUSHA MADAI YA UHURU KENYATTA YA KUNYIMWA HAKI ZA RAISI MUSTAAFU

SERIKALI YAKANUSHA MADAI YA UHURU KENYATTA YA KUNYIMWA HAKI ZA RAISI MUSTAAFU

  • Nairobi
  • Monday , Jun 10 , 2024
  • Last Updated June 10th, 2024 10:30pm
Serikali Yakanusha Kumnyima Uhuru Haki Yake Kama Rais Mstaafu

NA KHAMATI MWABAKA

MSEMAJI wa Serikali Isaac Mwaura amepuuzilia mbali taarifa ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwamba amenyimwa haki zake zikiwemo marupurupu kama inavyohitajika kisheria.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyumba vya habari Jumatatu jioni, Serikali kupitia kwa Bw Mwaura inasema imetekeleza matakwa yote ya Bw Kenyatta, ikiwemo kumnunulia magari na kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kinyume na alivyodai Msemaji wa Afisi ya Rais Mstaafu, Bi Kanze Dena, awali Jumatatu.

“Tumempa Bw Kenyatta jumla ya magari 14, na kinyume na madai kwamba hayalipiwi mafuta, rekodi zetu zinaonyesha kwamba juzi tu, Mei 15, 2024, magari hayo yalijazwa mafuta kupitia kwa kadi ya State House Master Card,” akasema Bw Mwaura.

Kuhusu madai ya kukataa kumkodishia afisi ya kuendesha shughuli zake kama rais mstaafu, Serikali inasema kwamba lazima Bw Kenyatta akubali kutumia jumba alilotumia aliyekuwa Rais Mstaafu, Hayati Mwai Kibaki kule Nyari.

“Hatuwezi kulipia kodi nyumba ya kibinafsi anayotumia kama ofisi, hiyo ni sawa na kukiuka sheria. Afisi aliyotumia Bw Kibaki kwa miaka tisa bado iko katika hali shwari kabisa na inafaa kwa Rais Mstaafu,” ikaendelea kusema taarifa hiyo.

© Copryright 2024 Intellectual posts All Rights Reserved

 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

soumis on
Rhys on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
Open chat
Chat On WhatsApp!
Hello
Can we help you?