Monday, April 20, 2026
spot_img
HomeCountiesWakoli Amnyoa Lusaka Bila Maji

Wakoli Amnyoa Lusaka Bila Maji

Seneta wa Kaunti ya Bungoma, David Wakoli……Picha/IP

ALEX WEKESA

Seneta wa Kaunti ya Bungoma, David Wakoli, ametoa mashambulizi makali dhidi ya serikali ya Gavana Kenneth Lusaka, akiituhumu kwa ukosefu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma.

Akizungumza na wanahabari katika ofisi yake mjini Bungoma, Wakoli alisema kuwa tangu mwaka wa kifedha 2023, kaunti hiyo imepokea zaidi ya KSh bilioni 40, lakini hakuna maendeleo yanayoendana na kiwango hicho kikubwa cha fedha kilichotumika.

Alisisitiza kuwa uongozi wa kaunti unapaswa kutoa taarifa ya kina kuhusu miradi iliyotekelezwa pamoja na manufaa yake kwa wananchi, akionya kuwa uwajibikaji na uwazi ni msingi muhimu wa matumizi sahihi ya rasilimali za umma.

Wakoli pia aliikosoa mabadiliko ya hivi karibuni katika baraza la mawaziri wa kaunti, akiyataja kama “mchezo wa paka na panya” unaotia shaka uthabiti wa uongozi na misingi ya utawala bora.

Alisema hatua ya kuwaondoa na kisha kuwarejesha au kuwahamisha mawaziri ndani ya muda mfupi inakwenda kinyume na matarajio ya wananchi na inadhoofisha imani kwa serikali ya kaunti.

Aliongeza kuwa baadhi ya maafisa waliorejeshwa tayari walikuwa wamependekezwa na Bunge la Kaunti kuondolewa kwa madai ya kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Miongoni mwao ni Carolyne Makali, aliyekuwa akihudumu katika Wizara ya Fedha.

Baada ya mabadiliko hayo, Makali alihamishiwa Wizara ya Barabara, huku Monica Fedha akipewa Wizara ya Miji. Bonventure Chengek aliteuliwa kuongoza Wizara ya Fedha, huku Naibu Gavana Janepher Mbatiany akichukua Wizara ya Biashara.

Wengine waliopangiwa majukumu mapya ni David Wamamili (Jinsia na Michezo), Agnes Wachiye (Elimu), Hebert Kibunguchy (Kilimo), Chrispinus Barasa (Afya) na Andrew Wamalwa (Maji).

Wakati huo huo, Douglas Sasita na Ben Emachar waliwekwa kwenye likizo ya lazima kufuatia mabadiliko hayo ya uongozi.

Wakoli alilitaka Bunge la Kaunti kuendeleza mchakato wa impeachment dhidi ya baadhi ya mawaziri waliopendekezwa kuondolewa, akisisitiza kuwa walishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha, alitoa changamoto kwa Gavana Lusaka kuchukua hatua kali za kusafisha na kurekebisha baraza lake la mawaziri ili kuhakikisha linahudumia wananchi kwa ufanisi na kurejesha imani ya umma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Recent Comments

soumis on
Rhys on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
WooCommerce on
Open chat
Chat On WhatsApp!
Hello
Can we help you?